Chama: 
SAU
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Satia Mussa Bebwa
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Hakushiriki uchaguzi
Idadi Ya kura: 
14 922

Muttamwega Bati Mgaywa (SAU)

Alizaliwa Februari 5, 1967 katika Hospitali ya Misheni Mwaibara, Bunda.

Mwaka 1975 Mgaywa alipokuwa na umri wa miaka nane alianza elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Igundu, Mwibara Bunda. Hapo alisoma darasa moja tu, kabla ya kuhamishiwa Shule ya Msingi Kibara Mwibara alikoendelea na darasa la pili mpaka alipohitimu darasa la saba mwaka 1981.

Mgaywa hakuendelea na sekondari badala yake, mwaka 1982 na 1983 alianza biashara kwa kusimamia miradi ya familia ya maroli na maduka yaliyokuwa Mwanza na Musoma.

Mwaka 1984, alijiunga na Shule ya Sekondari ya Shirati, Rorya kwa kidato cha kwanza hadi cha pili, kisha akahamia Sekondari ya Mugeza, Kagera alikohitimu kidato cha nne mwaka 1987.

Alijiendeleza katika kozi mbalimbali na amekuwa akiandika vitabu vya sayansi.