Chama: 
NRA
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Khamis Ali Hassan
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Hakushiriki uchaguzi
Idadi Ya kura: 
80 787

Leopard Mahona (NRA)

Alizaliwa Julai 4, 1978 katika kijiji cha Simbo mkoani Tabora. Alisoma shule ya Msingi Simbo na kuhitimu mwaka 1997. Mwaka 1998, alijiunga na Shule ya Sekondari Umoja, iliyopo Simbo Igunga alikosoma kidato cha kwanza mpaka cha nne na kuhitimu mwaka 2001.

Baada ya hatua hiyo hakuchaguliwa moja kwa moja kuendelea na ngazi inayofuata, hivyo aligeuka kuwa mchunga ng'ombe kwa miaka mitatu mfululizo.

Hata hivyo hakupoteza kiu yake ya kuendelea na masomo ambapo mwaka 2004 alianza masomo ya kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Yustino na alihitimu kidato cha sita mwaka 2006.

Mwaka 2011, ndoto yake ya kupata Shahada ya Chuo Kikuu ilitimia alipojiunga na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dar es Salaam.