Chama: 
DP
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Zaina Juma Khamis
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Hakushiriki uchaguzi
Idadi Ya kura: 
8 283

Philip John Fumbo (DP)

Fumbo alizaliwa Oktoba 10, 1970 Wilaya ya Kigoma Vijijini ambayo hivi sasa inaitwa Wilaya ya Uvinza.

Mwaka 1992 akiwa na umri wa miaka 22 ndipo alijiunga rasmi na harakati za kisiasa kupitia Chama cha Democratic Party (DP).

Lakini chama cha DP kilichelewa kupata usajili kwa sababu ya misimamo ya mwasisi wake, marehemu Christopher Mtikila, ya Utanganyika, inayopingana na Katiba. Kutopata usajili, Fumbo alijiunga na NCCR- Mageuzi, alikochaguliwa kuwa Katibu wa Wilaya ya Kigoma Vijijini kati ya Mwaka 1995 mpaka 2000.

Mwaka 2000 Fumbo alijiunga na TLP alikochaguliwa kuwa Katibu wa Wilaya hiyo hiyo mpaka mwaka 2005. DP ilipopata usajili Fumbo alirejea kwenye Chama hicho. Kati ya mwaka 2009 hadi 2019, alikuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mwakizega, Kigoma. Mwaka 2010 Fumbo aligombea Ubunge Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya DP lakini hakushinda, sasa anawania urais.