Chama: 
CCM
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Samia Suluhu Hassan
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Mshindi wa kiti cha urais (Kura 8,882,935)
Mshindi
Idadi Ya kura: 
12 516 252

Alizaliwa Oktoba 29, 1959 Wilayani Chato. Baada ya masomo yake ya elimu ya msingi na sekondari alijiunga na kozi ya ualimu ngazi ya Stashahada Mkwawa Iringa.

Kisha alihitimu masomo ya Shahada ya Kwanza ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1988. Mwaka 1994, alitunukiwa Shahada ya Uzamili ya Kemia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alifuzu shahada yake ya Uzamivu (PhD) ya Kemia Mwaka 2009, katika chuo hicho hicho. Amefanya kazi ya ualimu mkoani Mwanza mwanzoni mwa miaka ya 1980, kabla ya kuajiriwa na kampuni ya Nyanza kama mkemia wa kiwanda.

Mwaka 1995 alishinda ubunge jimbo la Chato. Kati ya mwaka 1995-2000, alikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi. Mwaka 2000-2005 alihudumia wizara mbili, Ardhi kisha Mifugo na Uvuvi. Mwaka 2010-2015, alikuwa Waziri wa Ujenzi. Mwaka 2015-2020, Rais wa Tanzania. Katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015 Dk. Magufuli alishinda kwa kupata kura 8,882,935  akifuatiwa na mgombea urais wa Chadema Edward Lowassa aliyepata kura 6,072,848.