Chama: 
ACT WAZALENDO
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Prof. Omar Fakih Hamad
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Hakushiriki uchaguzi
Idadi Ya kura: 
81 129

Bernard Membe (ACT-WAZALENDO)

Novemba 9, 1953 alizaliwa mwanasiasa huyo mkoani Lindi. Mwaka 1962, alijiunga na Shule ya Msingi Rondo-Chiponda Extended alikosoma kati ya mwaka 1962 na 1968.

Mwaka 1969 alijiunga na shule ya Seminari ya Namupa, iliyopo Lindi kwa masomo ya sekondari na alihitimu kidato cha nne mwaka 1972.

Kidato cha tano na sita alisoma shule ya Seminari ya Itaga, kisha alijiunga na masomo ya Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Na mwaka 1990 hadi 1992, Membe alisoma Shahada ya Uzamili ya Uhusiano wa Kimataifa, Chuo Kikuu cha John Hopkins, Washington DC, Marekani.

Mwaka 1978 alifanya kazi Ofisi ya Rais Mwaka 1992, aliteuliwa kuwa mshauri wa Balozi wa Tanzania nchini Canada. Mwaka 2000 alishinda ubunge jimbo la Mtama. Alishika unaibu waziri Mambo ya Ndani, Nishati na Madini na Waziri wa Mambo ya Nje.