Chama: 
CHADEMA
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Salum Mwalimu Juma
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Mshindi wa Ubunge jimbo la Singida Mashariki (kura 24,874)
Idadi Ya kura: 
1 933 271

Alizaliwa Januari 20, 1968 Wilayani Ikungi mkoa wa Singida. Alisoma katika Shule ya Msingi Mahambe, Singida kati ya mwaka 1976 na kuhitimu mwaka 1982.

Alijiunga na Sekondari ya Ilboru iliyopo Jijini Arusha kuanzia mwaka 1983 hadi 1986.

Mwaka 1987, alichaguliwa kuendelea na Shule ya Sekondari Galanos Tanga, kwa masomo ya kidato cha tano na sita. Mwaka 1989 alijiunga na mafunzo ya lazima ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Mwaka 1991, Lissu alianza masomo yake ya Shahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1994. Mwaka 1995 Lissu alipata ufadhili wa Serikali ya Uingereza kwenda kusoma Shahada ya Uzamili Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza na kumaliza masomo yake mwaka 1997.

Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa Mbunge Singida Mashariki hadi alipovuliwa ubunge mwaka 2019.