Rais Magufuli ala kiapo na kutoa ahadi

Alhamisi , 5th Nov , 2020

Rais mteule Dkt John Pombe Magufuli ameapishwa rasmi  kuwa Rais  wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania huku akiapa na kuahidi kuwatendea haki watu wote.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akila kiapo mbele ya Jaji mkuu wa Tanzania.

Magufuli  ameapishwa leo Novemba 5, jijini Dodoma pamoja na Makamu wake Samia Suluhu katika Uwanja wa Jamhuri na sherehe hiyo imehudhuriwa na Viongozi  kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Uganda ,Yoweri Museveni.

Katika kiapo chake , Rais Magufuli ameapa kuitetea, kuilinda na kuhifadhi katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kuahidi kutumika kwa uaminifu katika kazi zake za urais

Sherehe hii ya uapisho wa Rais Magufuli inampa tena nafasi nyingine ya kuiongoza Tanzania kwa muhula mwingine tena 2020- 2025 mara baada ya kupata ridhaa kwa watanzania.

Rais Magufuli alitangazwa kuwa Rais wa mteule wa Tanzania Oktoba 30 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kuongoza kwa kura 12, 516, 252 dhidi ya wapinzani wake 14.