Chama kwa Kirefu: 
Alliance for Change and Transparency
Chama Kilizaliwa: 
2014
Makao Makuu: 
Kijitonyama, Dar es Salaam
Mwenyekiti: 
Maalim Seif Sharif
Makamu Mwenyekiti: 
Dorothy Semu
Katibu Mkuu: 
Ado Shaibu
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
1
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
4

Ngao tatu za Ujamaa wa kidemokrasia (Democratic Socialism) kwa mujibu wa ACT-Wazalendo ni:

I)    Undugu ni hifadhi ya jamii ya asili kwa Afrika, na hivyo kila mtanzania na kila mwafrika ana jukumu la kumsaidia mwenzake anayekabiliwa na tatizo au janga popote alipo bila kutarajia malipo ya aina yeyote

II)    Serikali ina haki na wajibu wa kutengeneza sheria na kanuni zenye kulenga kuleta usawa wa kibinadamu katika jamii. Aidha, Serikali ina haki na wajibu wa kusimamia moja kwa moja sekta nyeti katika jamii zenye maslahi mapana ya kiusalama na kiuchumi kwa nchi

III)    Viongozi na watumishi wa umma wana wajibu wa kuhakikisha kwamba wanaishi na kuenenda katika misingi inayalinda heshima ya ofisi za umma na kwamba hawatumii nafasi zao kwa manufaa yao binafsi na jamaa zao.

Falsafa ya ACT Tanzania ni UNYERERE, ikiwa ni dhamira ya kurudisha, kuhuisha na kupigania misingi mama iliyoasisi Taifa la Tanzania, kama ilivyoanishwa katika Azimio la Arusha na kwa mazingira ya Tanzania ya sasa.
A)    Bendera ya Chama yenye rangi ya Zambarau, ambayo ndio alama kuu ya Chama. Rangi hii inawakilisha taswira ya mchanganyiko wa wanachama kutoka kona na pembe zote za nchi; utambuzi wa umuhimu wa wanawake na familia katika jamii; na alama ya kujali makundi yenye mahitaji maalum katika jamii wakiwemo watu wenye ulemavu, watoto na wazee.

B)    Bendera ya Taifa ikiashiria uzalendo, upendo na utayari wa kulilinda na kulitumikia Taifa la Tanzania.

C)    Mkono uliofunguka ukiashiria Uwazi.

Kiongozi wa chama hiki ni Bw. Zitto Zuberi Kabwe .

Mgombea Urais mwaka 2015 alikuwa Bi. Anna Mghwira na mwaka huu 2020 imemsimamisha Bwana Bernard Membe kama mgomea kiti cha urais