Makao Makuu: 
Buguruni Malapa, Dar es Salaam
Mwenyekiti: 
Hamad Rashid Mohamed
Katibu Mkuu: 
Doyo Hassan Doyo
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
0
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
0

Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimeanzishwa Agosti 28 mwaka 2012.  

Chama hiki kimejengwa katika misingi imara ya utu, uchaji wa Mungu na demokrasia ya haki. Ni chama ambacho kinalenga kuwajenga viongozi waadilifu kwa manufaa ya taifa kwa vizazi vyote.

Tofauti na vyama vingine nchini, ADC kinatambua na kuheshimu uwepo wa Mwenyezi Mungu. Huu ni mmoja ya misingi mikuu ya uongozi ndani ya ADC.

Chama cha ADC kinaamini kiongozi mwenye kumcha Mungu atakuwa mwadilifu na mwenye kutenda haki kwa wananchi.