Chama kwa Kirefu: 
Chama Cha Kijamii
Chama Kilizaliwa: 
2012
Makao Makuu: 
Ubungo, Dar es Salaam
Mwenyekiti: 
Constantine Akitanda
Katibu Mkuu: 
Renatus Muhabi
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
0
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
0

Chama Cha Kijamii (CCK), kilichoasisiwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Jamii (CCJ) kilichofutwa, kimepata usajili wa kudumu Januari 27 mwaka 2012 baada ya kutimiza masharti. 

CCK kinaamini katika kutekeleza wajibu wake Kikatiba kwa kuunganisha pamoja mawazo katika kushughulikia changamoto zote zinazoikabili nchi tangu baada ya Uhuru na kitakachobeba matarajio ya wananchi wa leo na kesho.

2015 Chama Cha Kijamii (CCK) hakijaweza kufanikiwa kusimamisha mgombea wa urais ila kimeweza kusimamisha wagombea mbalimbali wa nafasi ya ubunge na udiwani katika majimbo na kata mbalimbali nchini.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 CCK kimesimamisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais kwa upande wa Zanzibar.