Chama kwa Kirefu: 
Chama Cha Mapinduzi
Chama Kilizaliwa: 
1977
Makao Makuu: 
Dodoma
Mwenyekiti: 
Dk. John Magufuli
Makamu Mwenyekiti: 
Philip Mangula
Katibu Mkuu: 
Dk. Bashiru Ally
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
186
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
256

Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama tawala nchini Tanzania. CCM ilizaliwa 5 Februari 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala cha Zanzibar wakati huo.

Chama cha Mapinduzi kilikuwa kikiongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya Abeid Amani Karume. Kwa miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Itikadi hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha. Kutokana na azimio hilo uchumi uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hii pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.

CCM imekua ikiiongoza Tanzania bara na visiwani, huku ikishikilia rekodi ya kuwa na wabunge zaidi bungeni ambapo mwaka 2005 CCM iliandika historia kwa kushinda uchaguzi wa Raisi kwa kura 9,123,952 sawa na 80.28%.

Mwaka 2010 CCM ilishinda kwa kura 5,276,283 sawa na 62.83% ikiwa idadi ndogo ukilinganisha na mwaka uliopita