Chama kwa Kirefu: 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chama Kilizaliwa: 
1992
Makao Makuu: 
Kinondoni, Dar es Salaam
Kauli mbiu: 
People's Power
Mwenyekiti: 
Freeman Mbowe
Makamu Mwenyekiti: 
Tundu Lissu
Katibu Mkuu: 
John Mnyika
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
34
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
1

Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kilianzishwa mnamo tarehe 28 mwezi wa tano mwaka 1992, kufuatia mabadiliko ya mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania , kikiwa chini ya usimamizi wa aliyewahi kuwa Gavana wa Benki kuu Tanzania (BOT) Edwin Mtei huku makamu wa chama akiwa ni Brown Ngululuki

CHADEMA ilianzisha falsafa ya  NGUVU YA UMMA au "people's power" kikiamini umma kuwa sehemu ya serikali inayotoa ridhaa ya maamuzi na ruhusa ya mfumo wowote huku itikadi  ikiwa ni mlengo wa kati unaoamini katika soko huria lenye kusimamiwa.

Mwaka 1995 CHADEMA ilipata wabunge 4 na madiwani 42, mwaka 2000 ilipata wabunge 5 na Madiwani 75, mwaka 2005  walifanikiwa kuongeza idadi ya wabunge 6 na kufikia wabunge 11 na madiwani 103, mwaka 2010 waliandika historia kwakua upinzani wenye nguvu zaidi na kuongeza wabunge 31 hivyo kuwa na viti 49 katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na madiwani 467.

Katika uchaguzi wa Urais mwaka 2005 CHADEMA kupitia mgombea wake Freeman Mbowe walipata kura 688,756 sawa na asilimia 5.88%, lakini mwaka 2010 walimsimamisha Dr.Wilbroad Slaa na kupata jumla ya kura 2,271,491 sawa na asilimia 27.05%.