Chama kwa Kirefu: 
Civic United Front
Chama Kilizaliwa: 
1992
Makao Makuu: 
Buguruni Malapa, Dar es Salaam
Kauli mbiu: 
Haki sawa kwa wote
Mwenyekiti: 
Profesa Ibrahim Lipumba
Katibu Mkuu: 
Khalifa Suleiman Khalifa
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
32
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
3

CUF ilianzishwa mwaka 1992 kutokana na maungano ya shirika mbili. Hizi zilikuwa KAMAHURU kikundi cha kupambania demokrasia kwenye visiwa vya Unguja na Pemba Civic Movement iliyokuwa kundi la kupigania haki za binadamu la Tanzania bara.

CUF ilishiriki katika chaguzi za kitaifa pia za Kizanzibari. Ilifaulu vizuri kwenye visiviwa vya Zanzibar hasa Pemba lakini ilibaki hafifu Tanzania bara. Hata hivyo ni chama kikubwa cha upinzani katika bunge la Tanzania chenye wabunge 30 kati ya 324 kwa jumla.

Wimbo wa CUF unasema hivi: 
“Ni haki sawa kwa watu wote, kuendeleza taifa letu Utajirisho itikadi yetu, tukatae kuonewa. Siasa itumikie, uchumi wa Nchi yetu Ni mwiko huo uchumi, kutumikia siasa”