Chama kwa Kirefu: 
Democratic Party
Chama Kilizaliwa: 
2002
Makao Makuu: 
Mchikichini Ilala, Dar es Salaam
Mwenyekiti: 
Georgia Mtikila
Makamu Mwenyekiti: 
Dastan Malle
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
0
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
0

The Democratic Party (DP) ni chama cha upinzani nchini Tanzania kilichopata usajili wake tarehe 7 Juni 2002, kikiwa chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake Marehemu Christopher Mtikila.

Chini ya uongozi wa aliyekua Mwenyekiti wake Mchungaji Mtikila chama hiki kilijikita katika mapambano na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, katika kurekebisha mfumo wa utawala na kuboresha maendeleo ya Watanzania.

Umaarufu wa chama hiki uliongezeka zaidi pale ambapo kilitoa msimamo wake wa kuunga mkono hoja ya mgombea binafsi na kuiunga mkono hoja ya kuwa na seriakli tatu badala ya mfumo uliopo sasa nchini Tanzania wa serikali ya Mapinduzi.

Katika uchaguzi wa mwaka 2005 Marehemu Mchungaji Mtikila hakufanikiwa kuingia ikulu amabpo alipata asilimia 0.27% ya kura zote na kushika nafasi ya sita kati ya wagombea kumi, hali haikua nzuri kwa upande wa Zanzibar pia ambapo mgombea wa chama hiki katika nafasi ya Uraisi Bwana Abdallah Ali Abdallah alipata asilimia 0.11% jumla ya kura zote zilizopigwa.

 Juni, 2017 Chama cha Democratic Party (DP) kilimteua Georgia Mtikila kuwa mwenyekiti wa chama hicho kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa katiba