Chama kwa Kirefu: 
Demokrasia Makini
Chama Kilizaliwa: 
2001
Makao Makuu: 
Mabibo, Dar es Salaam
Mwenyekiti: 
Mohamed Ally Abdula
Katibu Mkuu: 
Ameir Hassan Ameir
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
0
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
0

Demokrasia MAKINI ni chama cha siasa kilichopata usajili wake rasmi tarehe 15 Novemba 2001. Makao Makuu yake yapo Mtaa wa Azimio, Mabibo Jijini Dar es Salaam.

Chama hiki kimetokana na kiu ya Watanzania kujiletea maendeleo ya hakika, haraka na ya kweli katika misingi ya kujitegemea, usawa, umoja na kuheshimu utu.

Pia kinatambua kuwa elimu bora hasa katika Sayansi ya Teknolojia, ndio njia pekee ya kuleta maendeleo ya uhakika na kweli kwa jamii ya Watanzania.