Chama kwa Kirefu: 
National Convention for Construction and Reform
Chama Kilizaliwa: 
1992
Makao Makuu: 
Ilala , Dar es Salaam
Kauli mbiu: 
UTU Itikadi Yetu
Mwenyekiti: 
James Mbatia
Makamu Mwenyekiti: 
Makamu Mwenyekiti
Katibu Mkuu: 
Elizabeth Martin Mhagama
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
1
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
0

NCCR-Mageuzi ni chama cha siasa kilichosajiliwa mnamo tarehe 29 Julai, 1992 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.  

Kwa mantiki ya jina lake Chama cha NCCR-Mageuzi kina mtazamo kwamba; Taifa la Tanzania linahitaji mageuzi katika mifumo mbalimbali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi inayotumika nchini; na kwamba taifa linahitaji kujengwa upya ili lifikie maendeleo makubwa katika nyanja zote; na kwamba, falsafa na itikadi sahihi, na sera madhubuti zinazosimamiwa na chama chenye nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi, ndizo zinazoweza kujenga nchi yenye uchumi imara, jamii iliyostawi vyema na taifa lenye amani ya kweli. Ni katika mtazamo huo, chama cha NCCR-Mageuzi kinafuata falsafa na itikadi ya kipekee inayowajali watu wote yaani; UTU.

Mwaka 1995 Chama kilimsimamisha ndugu A.L. Mrema kugombea urais. Mwaka 2000 Chama kilimsimamisha ndugu Edith S. Lucina kugombea urais. Mwaka 2005 Dkt. E.A. S. Mvungi aligombea urais na mwaka 2010 Chama kilimsimamisha ndugu Hashim S. Rungwe aligombea urais.Na katika mwaka wa 2015 chama kilijiunga katika Umoja wa Katiba ya Wananchi ambao unaviunganisha vyama vinne, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi pamoja na NLD, ambao kwa pamoja walisimamisha mgombea mmoja kwa tiketi ya CHADEMA akiwa chini ya mwamvuli wa UKAWA. Mh Edward Ngoyai Lowassa.

Mwaka 2020 kimesimamisha mgombe urais,