Chama kwa Kirefu: 
National Reconstruction Alliance
Chama Kilizaliwa: 
1993
Makao Makuu: 
Mtaa wa Bububu , Tandika Kilimahewa (Mtoni kwa Azizi Ali), Dar es Salaam
Mwenyekiti: 
Simai Abdulla
Katibu Mkuu: 
Hassan Kisabya
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
0
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
0

The National Reconstruction Alliance (NRA) ni moja ya vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu nchini Tanzania.

Mwaka huu NRA watawakilishwa na mgombea Uraisi Bwana Leopard Mahona. Huku moja kati ya sera zake kuu ikiwa ni kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa kuanzisha viwanda vya usindikaji bidhaa.

Mwaka 1995 chama hiki kilishiriki uchaguzi mkuu na kupata kura 60707 sawa na asilimia 0.94% ya kura zote lakini hakikufanikiwa kupata kiti chochote cha ubunge.

Mwaka 2000 chama hiki kilishiriki kwa mara nyingine tena uchaguzi mkuu bila mafanikio ambapo walipata kura 70 sawa na asilimia 0.00% ya kura zote zilizopigwa.

Na mwaka 2005 walishiriki tena uchaguzi mkuu bila mafanikio ambapo walipata kura 3459 sawa na asilimia 0.0% ya kura zote zilizopigwa.

Katika uchaguzi wa mwaka 2010 NRA hawakusimamisha mgombea katika kiti cha uraisi badala yake walimuunga mkono mgombea wa NCCR-MAGEUZI marehemu Dk. Sengondo Mvungi aliyepata asilimia 0.49% ya kura zote.

Mwaka 2015 mgombea Uraisi alikuwa Janken Kasambala