Chama kwa Kirefu: 
Sauti ya Umma
Chama Kilizaliwa: 
2005
Makao Makuu: 
Magomeni Kagera, Dar es Salaam
Mwenyekiti: 
Bertha Nkango Mpata
Katibu Mkuu: 
Majalio Paul Kyara
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
0
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
0

Sauti ya Umma (SAU) ni Chama cha Siasa Tanzania ambacho kilisajiliwa tarehe 17 Februari 2005. Makao

Makuu yake yapo Magomeni Kagera Jijini Dar es Salaam.

Madhumini ya SAU ni kukuza, kulinda na kutetea haki za binadamu na mkataba wa kimataifa inayolinda haki hizo na inayofutilia mbali ukandamizaji wa watu katika misingi ya rangi, jinsia, kabila, dini au tabaka.

Kuhakikisha kila mtu ana haki na uhuru wa kuabudu kwa minajili ya dini, madhehebu au imani yoyote anayotaka, bila ya kuathiri amani na utulivu wa jamii.