Chama kwa Kirefu: 
Tanzania Labour Party
Chama Kilizaliwa: 
1991
Makao Makuu: 
Magomeni-Usalama, Dar es Salaam
Mwenyekiti: 
Augustine Lyatonga Mrema
Makamu Mwenyekiti: 
Joas Kayura
Katibu Mkuu: 
Dominata Rwechungura
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
0
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
0

TLP ilitokea mapema mwaka 1991 kutokana na mwelekeo wa dunia, ambako mageuzi yalikuwa yameshika kasi Tanzania. Leo Lwekamwa, Mwasisi wa Chama cha Tanzania Labour (TLP). Ni Mwenyekiti wa Kwanza wa chama hicho cha upinzani kilichojizolea umaarufu mkubwa wakati wa Uchaguzi wa Pili wa mfumo wa vyama vingi nchini uliofanyika mwaka 2000.

Tanzania Labour Party (TLP) inaamini kwamba mkulima, mvuvi, mfugaji au mtu wa kuchimba madini wote ni wafanyakazi kwa kuwa wanatoka jasho ili kupata riziki. Hata mfanyakazi wa ofisini anatumia akili ambako anatoka jasho. Wote ni wafanyakazi ambao wanastahili kukombolewa kiuchumi. 

Mwaka 1999 ilimpokea Augustine Lyatonga Mrema na kuwa Mwenyekiti wa TLP na mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka (2000) ,Mwaka 2005 TLP ilimteua tena Augustine Lyatonga Mrema kugombea nafasi ya urais na aliweza kupata kura 84,901 sawa na asilimia 0.75, kwa mwaka 2010 TLP ilimteua Mgaywa Muttamwega Bhatt kugombea nafasi ya urais na matokeo alipata kura kura 17,482 sawa na silimia 0.20.

2015 TLP imemteua Macmillan Elifatio Lyimo kugombea nafasi ya urais.