Chama kwa Kirefu: 
United Democratic Party
Chama Kilizaliwa: 
1992
Makao Makuu: 
Mtaa wa Ilemela Mwananyamala, Dar es Salaam
Mwenyekiti: 
John Cheyo
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2015): 
0
Viti vya Ubunge (Uchaguzi 2020): 
0

Chama hiki kilianzishwa mwaka 1992 na kupata usajili wake rasmi mwaka huo huo.

Mwenyekiti wa chama hiki anaitwa John Cheyo, ambaye amewahi kuwa mbunge wa Bariadi Mashariki kuanzia mwaka 2005 mpaka mwaka 2010.

Chama hiki kimeshiriki uchaguzi mkuu katika vipindi tofauti, mwaka 1995 kilimsimamisha mgombea uraisi John Cheyo ambaye alipata kura 25874 sawa na asilimia 3.97% ya kura zote, katika nafasi ya ubunge chama hiki kilijipatia kura 213547 sawa na asilimia 3.32% ya kura zote, ambapo kilipata nafasi 2 za uwakilishi bungeni.

Katika, uchaguzi wa mwaka 2000 chama hiki kilipata kura 342891 sawa na asilimia 4.20% katika nafasi ya uraisi, katika nafasi ya ubunge kilipata kura 315303 sawa na asilimia 4.44% na kufanikiwa kutetea nafasi zake mbili za ubunge.

Uchaguzi wa mwaka 2005 chama hiki hakikufanikiwa kusimamisha mgombea wa Uraisi na badala yake kilisimamisha wagombea ubunge na kupata kura 155887 sawa na asilimia 1.4% ambapo walifanikiwa kupata kiti kimoja tu cha ubunge.

Katika uchaguzi wa mwaka 2010 chama hiki hakikufanya vizuri sana lakini kilifanikiwa kupata nafasi moja ya ubunge wa kuteuliwa.

Katika uchaguzi wa mwaka huu chama hiki hakijasimamisha mgombea yoyote katika nafasi ya uraisi.