AAFP yaahidi kuwatolea mahari vijana Zanzibar

Jumatatu , 19th Oct , 2020

Mgombea Urais Zanzibar, kupitia Chama cha Wakulima (AAFP), Said Soud Said, amesema endapo atapa rufaa ya kuiongoza Zanzibar atahakikisha serikali inatoa mahari kwa vijana ili waoe.

Mgombea Urais Zanzibar, kupitia Chama cha Wakulima (AAFP), Said Soud Said

Akizungumza na wananchi visiwani humo Said Soud, amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kutatua  na kuliondoa tatizo la ubakaji kwenye jamii katika visiwa hivyo.

“Pindi nikipata rufaa yakuiongoza Zanzibar, nawaahidi vijana wote kwamba mtaoa na mahali itatolewa na serikali ili kuondosha tatizo la ubakaji, kwa vile unataka kuoa utakuja wewe serikalini na serikali itakupa pesa itakushughulikia harusi yako hiyo utaondoka” alisema Said Soud Said.

Aidha mgombea huyo amesema kuwa wananchi wanahitaji kusoma ili kuweza kuijenga nchi yao ambapo ameahidi  kuwawezesha vijana kupata elimu ya viwanda ili kuongeza ujuzi na kusaidia kuanzisha viwanda kwa ajili ya kukuza uchumi nchi.