Lipumba atangaza kufunga bila kula siku ya Alhamis

Jumatatu , 2nd Nov , 2020

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ametangaza kuwa kutokana na uchaguzi mkuu ulivyoendeshwa nchini, chama hicho hakitashiriki uchaguzi wowote.

Lipumba ameyasema hayo leo Novemba 2, 2020 makao makuu ya ofisi hizo,  jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kuwa sasa watajikita katika harakati za kudai katiba mpya, ili kupatikana kwa Tume huru ya Uchaguzi.

“CUF tunawaomba watanzania wote wapenda haki kuungana na sisi katika ibaada siku ya Alhamis, ambapo tutafunga kwa kutokula mchana na tufanye dua na maombi kila mmoja kwa imani yake ili kuomba hukumu ya haki kutokana na kile kilichofanyika”- Prof. Lipumba.

Aidha Lipumba ameongeza kuwa  “Hatukubaliani na matokeo kwasababu tumeibiwa sana, mfano Jimbo la Temeke mgombea wetu wa Ubunge katika kituo alichopiga kura yeye na familia yake amepata kura sifuri ina maana hata mwenyewe hakujichagua”.