Together Tunawakilisha
Home

YOU ARE NOT LOGGED IN
  • Login
  • or
  • Sign Up
  • Dashboard
  • Logout
  • Home
  • Shows
  • News
    • Currrent Affairs
    • Entertainment
    • Sport
    • Business
    • Life & Style
  • Gallery
  • Schedule
  • Namthamini
  • Wanafunzi wa shule ya sekondari Kyanyari wakipokea taulo za kike

    Wanafunzi wa kike 800 wapatiwa taulo za kike Mara
    Wilaya mbili za Musoma na Butiama kila wilaya ilipokea taulo za kike 400
  • Balozi wa kampeni ya Namthamini, Justine Kessy akizungumza na Meneja Rasilimali watu wa ITV, Bi. Hellen Elipokea wa katikati.

    ITV wachangia Namthamini pakiti 1200
    Ambazo zinaweza kuwasaidia wanafunzi 100 kwa mwaka mzima
  • Balozi wa kampeni ya Namthamini, Justine Kessy akipokea taulo za kike kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Luna Pads, Luna Kikuchi.

    Luna Pads wamthamini mtoto wa kike
    Wamechangia taulo za kike pakiti 50 ili kumbakisha binti shuleni
  • Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbambi akipokea zawadi ya t-shirt ya Namthamini.

    Namthamini 2022 wanafunzi wamepata zawadi kibao
    Wamepatiwa taulo za kike na elimu ya hedhi salama
  • Namthamini 2022 wanafunzi wamepata zawadi kibao
    Wamepatiwa taulo za kike na elimu ya hedhi salama

Wasichana

kutoka mikoa zaidi ya 15 Tanzania wamenufaika

Msaada wa Pesa

Changia kiasi chochote cha pesa
5,000/=
(Je wajua kwa TZS 5,000/= inamweka mtoto wa kike shule mwezi mzima?)
Changia (Donate)
Toa mchango wako wa Fedha kwa njia zifuatazo
1
Bank
Akaunti Namba: 015043198200
Jina la Account: Namthamini
Jina la Benki: CRDB
2
MPESA
Unaweza kuchangia kwa namba ya malipo 5999900
jina East Africa Television
Kwa mawasiliano zaidi piga 0787 633 313

Changia Pedi

Changia pedi kumsaidia binti mmoja kwa mwaka.
Changia (Donate)
Wasilisha mchango wako wa PEDI
Ofisi za East Africa Television na East Africa Radio, Mikocheni, Dar es salaam.
Kwa mawasiliano zaidi piga 0787 633 313
Habari

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Lukosi Wilayani Kilolo Iringa wakipokea msaada wa pedi.

Wasichana Sekondari Iringa waishukuru Namthamini

Kampeni ya NAMTHAMINI inayoendeshwa na East Africa Television na East Africa Radio kwa mwaka wa...

Soma zaidi

Wasichana Sekondari Iringa waishukuru Namthamini

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Lukosi Wilayani Kilolo Iringa wakipokea msaada wa pedi.

Baadhi ya wanafunzi katika shule tofauti tofauti za wilayani Kilolo, wamesema kuwa ukosefu wa taulo hizo za kike imekuwa ni moja ya changamoto inayowafanya baadhi yao hasusani wanaotoka familia duni kushindwa kuhudhuria masomo kikamilifu, wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.

Anifa Athumani ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Lukosi ambayo ilipokea msaada wa zaidi ya pakiti 3568, amesema sasa tatizo la kukosa masomo limetatuliwa.

Kwa upande wake Shaila Musa, mwanafunzi wa Sekondari Mazombe ambayo imenufaika kwa kupata pakiti 2640 za pedi, amekiri kupitia changamoto ya kukosa masomo wakati wa hedhi hivyo kupitia Namthamini ataweza kusoma kwa mwaka mzima.

Mwakilishi wa East Africa Television na East Africa Radio Deogratius Kithama, akikabidhi msaada wa pedi katika shule ya Sekondari Lukosi wilayani Kilolo mkoani Iringa wiki iliyopita. Pedi hizo zimetokana na Kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na vituo hivyo kwa mwaka wa nne mfululizo, ambapo kwa Iringa imezifikia shule tatu za Sekondari ambazo ni Lukosi Sekondari, Mazombe Sekondari na Nyalumbu Sekondari.

Shule nyingine ambayo imepata pedi zaidi ya pakiti 1604, ni Nyalumbu ambapo mwanafunzi Theresia Richard, ameishukuru East Africa Television na East Africa Radio na kuahidi watajituma zaidi ili wafaulu.

Kwa upande wake Antokiye Kivanda ambaye ni mwalimu wa malezi katika shule ya Sekondari Mazombe ameeleza hali ilivyo katika shule hiyo kuwa changamoto ya pedi kwa wasichana ni kubwa hivyo msaada uliotolewa utawasaidia kuongeza mahudhurio kwa wanafunzi.

Aidha akizungumza na timu ya East Africa Television na East Africa Radio ofisini kwake, Afisa Elimu Mkoa wa Iringa Aloyce Kamamba ameeleza kufurahishwa na kampeni hiyo huku akiomba izidi kuongeza idadi ya shule mkoani humo kwa mwaka ujao.
 

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo (katikati) akipokea taulo za kike. Kushoto ni Mtangazaji TBway na kulia ni Deogratius Kithama.

Jokate aipokea Namthamini, wanafunzi wanufaika

Zoezi la ugawaji wa pedi kwa wanafunzi wa kike katika shule mbalimbali nchini kupitia kampeni...

Soma zaidi

Jokate aipokea Namthamini, wanafunzi wanufaika

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo (katikati) akipokea taulo za kike. Kushoto ni Mtangazaji TBway na kulia ni Deogratius Kithama.

Shule hizo ni Kibuta Sekondari ambayo ilipatiwa jumla ya pakiti 804 kwaajili ya wanafunzi 80 na watatumia kwa zaidi ya mwaka mmoja, hivyo kuwa na uhakika wa kutokosa masomo kwa changamoto ya kukosa pedi wakati wa hedhi.

Shule ya pili ni Maneromango Sekondari ambayo ilipatiwa jumla ya pakiti 1086 kwaajili ya 108, ambayo pia watakuwa na uhakika wa kuwa na taulo za kike kwa mwaka mzima.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, alishiriki kupokea taulo hizo katika shule zote akiwa ameambatana na timu ya East Africa Television na East Africa Radio.

Baada ya kupokea taulo hizo Mh Jokate aliwasihi wanafunzi kuona kama ni nafasi ya kujituma kwenye masomo ili kuwapa motisha watu waliochangia kuweza kuwasaidia tena.

'East Africa TV na East Africa Radio ni kampuni kubwa sana, wameacha kazi zao kwaajili ya kuja kuwathamini nyie, kwahiyo mnatakiwa muwalipe kwa kujituma na kufanya vizuri kwenye masomo yenu ili warudi tena', alisema Jokate.

Aidha Jokate aliishukuru East Africa Television na East Africa Radio kwa kuweka wazi kuwa zimemsaidia katika kampeni yake ya Tokomeza Zero Kisarawe kwa kutoa pedi hivyo kupunguza tatizo la utoro kwa wanafunzi wa kike wanapokuwa katika hedhi.
 

Baadhi ya wanafunzi na walimu mkoani Mbeya

Kampeni ya Namthamini yaleta faraja Mbeya

Kampeni ya Namthamini,  inayoratibiwa na East Africa Television na East Africa Radio yenye...

Soma zaidi

Kampeni ya Namthamini yaleta faraja Mbeya

Baadhi ya wanafunzi na walimu mkoani Mbeya

Kampeni hiyo ya Namthamini imezifikia Shule tatu za Sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya  ambazo ni Nsenga, Stellafarm pamoja na Maziwa na kuzungumza na mabinti ambao walieleza changamoto zinazowakabili wanapokuwa kwenye hedhi na namna ambavyo taulo za kike zitawasaidia kuondokana na vikwazo wawapo shuleni.

Walimu wa shule zilizonufaika na msaada wa pedi  wameiomba EATV kuendelea kuzisaidia shule hizo, kwani uhitaji bado ni mkubwa.

Akizungumza kwa niaba ya Ofisa Elimu Sekondari Jiji la Mbeya, Hope Mariki amesema jumla ya Wanafunzi 379  wa kike kutoka Shule za Nsenga, Stellafarm na Maziwa wamenufaika na taulo hizo za kike.

Ni miaka mitatu sasa tangu East Africa Television na East Africa Radio, zianzishe  kampeni ya Namthamini yenye kauli mbiu isemayo Namthamini Nasimama Naye ambapo imefika katika mikoa mbalimbali nchini.

Kwa mwaka 2019 pekee tayari imefika katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Dodoma, Tabora na Manyara na kugusa zaidi ya wanafunzi 5000.
 

  • Tazama zaidi

Namthamini

  • English
Kampeni
Namthamini

Mwaka 2017 East Africa Television LTD ilianzisha kampeni ya kuchangisha taulo za kike kwa wanafunzi wenye uhitaji shuleni. 

Kampeni hii ilikuja baada ya tafiti kuonesha kuwa wasichana wengi hupata changamoto katika siku zao za hedhi kwa kushindwa kununua taulo za kike hivyo kupelekea kukosa masomo shuleni kwa takribani siku 3 mpaka 7 kwa mwezi za masomo. 

2024 ni mwaka wa saba (8) tangu kuanzishwa kwa mradi huu, tukishiriana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) lengo kuu likiwa ni kuhakikisha watoto wa kike wanapata sio tu taulo za kike lakini pia wanakuwa na vyoo vizuri na maji safi mashuleni ili wabaki salama katika siku zao za hedhi.

Mwaka huu 2024, kampeni hii ina lengo la kufikia watoto wa kike 10,000 katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania.

Lengo la Kampeni
Lengo letu kuu ni kumsaidia msichana huyu kwa kumpatia taulo salama na kuhakikisha hakosi tena masomo yake na anafikia ndoto zake.

'Unapomuinua mtoto mmoja wa kike, umeinua jamii nzima' 
#Namthamini 
#NasimamaNaye

Shule Nufaika
Arusha
Shule ya Sekondari Arusha
Arusha
Shule ya Sekondari Arusha
Arusha
Shule ya Sekondari Kinana
Arusha
Shule ya Sekondari Muriet
Arusha
Shule ya Sekondari Musa
Arusha
Shule ya Sekondari Ngarenaro
Bukoba
Shule ya Sekondari Izimbya
Bukoba
Shule ya Sekondari Ruhunga
Dar es salaam
Shule ya Msingi Rahaleo
Dar es salaam
Shule ya Msingi Tuliani
Dar es salaam
Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Abdu Jumbe
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Buza
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Jangwani
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Kibugumo
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Kidete
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Kisota
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Kisutu
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Maendeleo
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Minazini
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Tungi
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Turiani
Dar es salaam
Shule ya Sekondari Twiga
Dodoma
Shule ya Sekondari Hombolo
Dodoma
Shule ya Sekondari Kikombo
Dodoma
Shule ya Sekondari Msalato
Iringa
Shule ya Sekondari Lukosi
Iringa
Shule ya Sekondari Mazombe
Iringa
Shule ya Sekondari Nyalumbu
Kigoma
Shule ya Sekondari Bogwe
Kigoma
Shule ya Sekondari Katubuka
Kigoma
Shule ya Sekondari Kigoma Grand
Kigoma
Shule ya Sekondari Mlole
Kigoma
Shule ya Sekondari Murubona
Kigoma
Shule ya Sekondari Mwananchi
Lindi
Shule ya Sekondari Mchinga
Lindi
Shule ya Sekondari Ngongo
Manyara
Shule ya Sekondari Simbay
Manyara
Shule ya Sekondari Sumaye
Mara
Shule ya Msingi Mwisenge
Mara
Shule ya Sekondari Kyanyari
Mbeya
Shule ya Sekondari Busokelo
Mbeya
Shule ya Sekondari Garijembe
Mbeya
Shule ya Sekondari Kalonge
Mbeya
Shule ya Sekondari Maziwa
Mbeya
Shule ya Sekondari Nsenga
Mbeya
Shule ya Sekondari Stellafam
Mbeya
Shule ya Sekondari Usongwe
Mtwara
Shule ya Sekondari Chiungutwa
Mtwara
Shule ya Sekondari Lukuledi
Mtwara
Shule ya Sekondari Mangamba
Mtwara
Shule ya Sekondari Masasi
Mtwara
Shule ya Sekondari Mikindani
Mtwara
Shule ya Sekondari Mitengo
Mtwara
Shule ya Sekondari Naliendele
Mtwara
Shule ya Sekondari Nanyumbu
Mtwara
Shule ya Sekondari Napacho
Njombe
Shule ya Sekondari Iwawa
Njombe
Shule ya Sekondari Kitulo
Njombe
Shule ya Sekondari Mabatini
Njombe
Shule ya Sekondari Mavala
Njombe
Shule ya Sekondari Mchuchuma
Pwani
Shule ya Sekondari Dunda
Pwani
Shule ya Sekondari Kibuta
Pwani
Shule ya Sekondari Maneromango
Pwani
Shule ya Sekondari Matimbwa
Ruvuma
Shule ya Sekondari Luwawasa
Ruvuma
Shule ya Sekondari Manyanya
Ruvuma
Shule ya Sekondari Mashujaa
Ruvuma
Shule ya Sekondari Mbambi
Ruvuma
Shule ya Sekondari Mbinga
Shinyanga
Shule ya Sekondari Kishapu
Shinyanga
Shule ya Sekondari Mwataga
Shinyanga
Shule ya Sekondari Samuye
Shinyanga
Shule ya Sekondari Tinde
Simiyu
Shule ya Sekondari Badi
Simiyu
Shule ya Sekondari Binza
Simiyu
Shule ya Sekondari Kidinda
Simiyu
Shule ya Sekondari Somanda
Singida
Shule ya Sekondari Gunda
Singida
Shule ya Sekondari Ntuntu
Tabora
Shule ya Sekondari Idete
Tabora
Shule ya Sekondari Ikomwa
Tabora
Shule ya sekondari Ndono
Tabora
Shule ya Sekondari Tura
Tanga
Shule ya Sekondari Korogwe
Tanga
Shule ya Sekondari Kwamatuku
Tanga
Shule ya Sekondari Kwedzinga
Tanga
Shule ya Sekondari Segera
Yaliyosemwa
  • "Rotary tulianzisha mradi wa kuwawesha mabinti katika masuala ya hedhi, club zote nchini zinaelimisha wavulana kwa wasichana kuhusu hedhi salama kwa kushirikiana na wadau wetu kama kampeni ya Namthamini"
    Aisha Sykes
    Rotary Oysterbay
    Rais wa Rotary Oysterbay
  • “Nawashukuru sana kwa namna ambavyo mnahudumia jamii ya watoto wa Tanzania, asanteni kwa huduma mnayoifanya kwa watoto wetu”
    Rosalia Mwita
    Twiga Sekondari
    Mkuu wa Shule
  • ''Nawapongeza East Africa TV na Radio kwa jitihada zao katika Kampeni hii na mimi na naungana nao, tuendelee kuwa pamoja katika hili ili tuweze kuwasaidia mabinti zetu na tuzalishe viongozi wa kike wengine wazuri katika siku za baadae'' - Mh. Fatma Nyangasa
    Fatma Nyangasa
    Wilaya ya Kigamboni
    Mkuu wa Wilaya
  • "Kuhusu kampeni ya #Namthamini mimi mwenyewe nimeshiriki kuongea na wazazi kuhusu umuhimu wa kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu na anatimiza ndoto zake".
    Thobias Andengenye
    Kigoma
    Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
  • 'Nawashukuru kwa kuja na wazo hili la kampeni ya #Namthamini hili litamsaidia mtoto wa kike kuwa huru na kuondoa tatizo kutohudhuria masomo pindi wanapokuwa katika hedhi''
    Dollah Kusenge
    Kasulu
    Mkurugenzi wa Wilaya ya Kasulu
  • 'Hatutaki mtoto wa miaka 6 afikirie kuwa Mwali, afikirie kuchezwa ngoma tunataka afikirie kusafirisha Cherry tomato nje ya nchi' - Mh. Jokate Mwegelo
    Jokate Mwegelo
    Wilaya ya Kisarawe
    Mkuu wa Wilaya

ABOUT US

  • About us
  • Advertise
  • Jobs
  • Terms & Conditions
  • Contact Us
  • Frequently Asked Questions

Network

  • IPP MEDIA
  • EAST AFRICA RADIO
  • ITV
  • RADIO ONE
  • CAPITAL RADIO
  • LOKOPROMO

©  East Africa Television Limited. All Rights Reserved

  • Main menu
    • Home
    • Shows
    • News
      • Currrent Affairs
      • Entertainment
      • Sport
      • Business
      • Life & Style
    • Gallery
    • Schedule
      • Awards
      • BBALLKINGS
      • Dance100
    • Namthamini
  • Search
  • Main menu
    • Home
    • Shows
    • News
      • Currrent Affairs
      • Entertainment
      • Sport
      • Business
      • Life & Style
    • Gallery
    • Schedule
      • Awards
      • BBALLKINGS
      • Dance100
    • Namthamini
  • Search